Faraja Yangu TV ni jukwaa la televisheni la Kiislamu linalolenga kuleta elimu, mawaidha, na burudani ya dini ya Kiislamu moja kwa moja nyumbani kwako. Tunatoa vipindi mbalimbali vya dini, mawaidha, qaswida, maulidi na nyimbo za kiroho kwa ajili ya familia nzima.
Ndiyo! Programu ya Faraja Yangu TV ni bure kabisa. Unaweza kuisakinisha kutoka kwenye Google Play Store na kuanza kutazama maudhui yetu mara moja. Hakuna malipo yoyote ya kila mwezi au mwaka.
Programu yetu inafanya kazi kwenye simu zote za Android zenye mfumo wa Android 5.0 (Lollipop) na zaidi. Pakua programu yetu kutoka kwenye Google Play Store.
Video zetu zina muda tofauti kulingana na aina ya maudhui. Mawaidha na mihadhara kwa kawaida ni dakika 30-60, qaswida ni dakika 5-15, na vipindi vya elimu ni dakika 20-45.
Ndiyo! Programu yetu ina kipengele cha kupakua video (download) ili uweze kutazama video bila mtandao. Unahitaji coin za ndani ya programu ili kupakua video. Coin hutolewa baada ya kuangalia matangazo.
Unapata coin kwa kuangalia matangazo ndani ya programu. Kila tangazo moja lina thamani ya coin 10. Unaweza kutumia coin kupakua video kwa matumizi ya nje ya mtandao (offline).
Unaweza kubook shughuli yako moja kwa moja kwenye tovuti yetu kupitia sehemu ya Packages na Booking. Chagua package unayopenda, jaza fomu, na ulipe asilimia 70 ya gharama kama kianzio. Pia unaweza kuwasiliana nasi kupitia WhatsApp.
Maudhui yetu yanajumuisha: Mawaidha ya dini, Qur'an na Tajweed, Qaswida za Kiswahili, Maulidi barazanji, Swifat Rasoul, Mihadhara ya kiislamu, na vipindi vya vijana. Tunatoa maudhui ya familia nzima.
Unaweza kuwasiliana nasi kupitia:
📧 Barua pepe: farajamobile@gmail.com
📱 Simu: +255 699 529 291
💬 WhatsApp: +255 699 529 291
📍 Anwani: Dar es Salaam, Tanzania
Ndiyo! Tuna utangazaji wa moja kwa moja (live streaming) 24/7. Unaweza kuangalia live kwenye tovuti yetu au ndani ya programu kwa kubonyeza kitufe "MOJA KWA MOJA".